July 4, 2016


Baada ya kupoteza michezo yake miwili dhidi ya Mo Bejaia na TP Mazembe, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm ametamka kuwa ni lazima kwa kikosi chake kuibuka na ushindi mbele ya Medeama kwa sababu timu hiyo anaijua vema tangu alipokuwa nchini Ghana.

Yanga inatarajia kuvaana na Medeama ya Ghana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Pluijm amesema tayari ana ufahamu wa kila kitu juu ya wapinzani wao, Medeama wanavyocheza pamoja na mbinu zao baada ya kupewa ripoti walipocheza na TP Mazembe, wiki kadhaa zilizopita ambapo jambo hilo anaona litamsaidia kuhakikisha anaibuka na pointi hapa na kuanza kufufua matumaini ya kusonga mbele. 

“Lazima tushinde mbele ya Medeama kwa ajili ya kufufua matumaini yetu ya kutinga nusu fainali na hilo linawezekana kwa sababu tayari maelezo yote yatakayotupa pointi dhidi yao, tunayo.

“Tunawajua namna wanavyocheza baada ya kupokea ripoti wakati tulipowafanyia uchunguzi walipocheza na TP Mazembe, jambo ambalo naamini litakuwa msaada mkubwa kwetu.

“Lakini klabu hii naifahamu tangu nilipokuwa Ghana na najua timu nyingi za huko zinavyocheza jambo ambalo linazidi kutupa na kutuweka katika mazingira mazuri ya kushinda lakini kikubwa ambacho tunatakiwa kukifanya ni kujiandaa vyema,” alisema Pluijm.

Medeama imecheza mechi mbili, ina pointi moja baada ya kufungwa mabao 3-1 na TP Mazembe kisha ikatoka suluhu dhidi ya MO Béjaïa, wakati Yanga haina pointi, hivyo ushindi pekee ndiyo ambao unaweza kuiamsha Yanga kutoka usingizini katika michuano hiyo.


Kundi A
                              P    W    D     L     Pts
1. TP Mazembe       2     2     0     0     6
2. MO Béjaïa           2     1     1     0     4
3. Medeama            2     0     1     1     1

4. Yanga                 2     0      0     2     0

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV