September 27, 2016


Serge Wawa sasa yuko tayari kuanza kukichezea kikosi cha Azam FC, lakini suala la majeruhi linaonekana kuwa tatizo kwao.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema Wawa amerejea na sasa mwalimu anaweza kumtumia. Lakini akasisitiza, majeruhi mfululizo yamewavuruga, hasa katika safu ya ulinzi.

“Kweli Wawa amerejea, sasa hili tunamuachia mwalimu mwenyewe ataamua kama anamtumia au la,” alisema.

“Safu ya ulinzi imekuwa ikiandamwa na majeruhi mfululizo. Mfano Wawa alikuwa majeruhi, Aggrey pia, Erasto Nyoni naye ni majeruhi. Utaona hili ni tatizo kubwa.

Mechi inayofuata ya Azam FC ni dhidi ya Ruvu Shooting na itaingia uwanjani wikiendi ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ndanda FC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV