September 27, 2016


Mganda Hamisi Kiiza ameshindwa kuisaidia timu yake ya Free State Stars ambayo inaonekana kwenda mwendo wa kobe kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Free State tayari imecheza mechi tano za ligi hiyo na haijashinda mechi hata moja, ikiwa imepoteza ttau na sare mbili tu.

Katika mechi hizo, mbili imecheza nyumbani na moja imepata sare na moja imefungwa huku ikiwa imepoteza mbili nyingine ugenini na kuambulia sare moja dhidi ya SuperSport United.

Kiiza ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu, hajaonyesha cheche zozote licha ya kwamba msimu uliopita alikuwa katika nafasi ya pili wakati akiichezea Simba baada ya kufunga mabao 19 na kuwa nyuma ya Amissi Tambwe aliyeibuka mfungaji bora.

Kesho, timu hiyo inarejea uwanjani tena, safari hii inakutana na magwiji wa Soweto na vigogo wa Afrika Kusini, Kaizer ‘Iwiza’ Chiefs.

Free State ndiyo timu aliyovunja mkataba Mtanzania, Mrisho Ngassa ambaye ametimkia Oman na kujiunga na klabu ya Fanja.

MECHI TANO:
Cape Town City 1 - 0 Free State Stars
Chippa United 2 - 1  Free State Stars
Free State Stars 0 - 0 Bloemfontein Celtic
Free State Stars 0 - 1 Golden Arrows

SuperSport United 0 - 0  Free State Stars

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV