November 14, 2017




Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amerejea nchini akitokea kwao nchini Zambia.

Lwandamina alikwenda Zambia kuhani msiba wa mdogo wake ambaye alifariki naye akashindwa kwenda kwenye mazishi kutokana na kubanwa na majukumu.

Awali, Lwandamina alikuwa arejee nchini jana usiku, lakini ikashindikana hadi alipotua leo alfajiri.

Hata hivyo, kutokana na uchovu, Lwandamina ameshindwa kuanza mazoezi na kikosi cha Yanga hadi kesho.

“Kweli kocha amefika, lakini atakuwa amechoka sana kwa kuwa amefika alfajiri hii,” kilieleza chanzo.


Kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi ya uwanjani leo baada ya mapumziko ya siku mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic