January 25, 2018


Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi yake chini ya Kocha mpya, Pierre Lechantre.
Lechantre raia wa Ufaransa, ameiongoza Simba siku yake ya pili kazini akisaidiwa na wasaidizi wawili, Masoud Djuma na Mohamed Habibi.

Kwa siku ya pili mfululizo mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.


Simba inajiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara, mara ya mwisho wameibugisa Kagera Sugar mabao 2-0 kwao Kagera.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic