January 25, 2018


Mashabiki zaidi wamejitokeza kuishuhudia Simba ikijifua chini ya Kocha mpya, Peirre Lechantre raia wa Ufaransa.


Simba inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.

Mara ya kwanza, Lechantre akisaidiana na Mohamed Habibi kutoka Tunisia na Masoud Djuma kutoka Burundi alianza rasmi kuifundisha Simba, jana.


Leo ameendelea huku idadi ya mashabiki ikilinganishwa na ile ya jana ikiongezeka.

Simba inajiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara, mara ya mwisho wameibugisa Kagera Sugar mabao 2-0 kwao Kagera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic