January 25, 2018


Beki mkongwe wa kati wa Lipuli FC, Joseph Owino anatarajia kurejea mazoezini kesho atakapoanza kukimbia mdogomdogo.

Owino aliumia na kulazimika kushonwa nyuzi saba mdomoni wakati Lipuli FC ikiivaa Mbeya City.

Taarifa za viongozi wa Lipuli FC ilionyesha kwamba Owino alipigwa kiwiko na kujeruhiwa vibaya mdomoni.

Msemaji wa Lipuli FC, Clement Sanga amesema Owino ambaye amesafiri na kikosi hicho hadi mjini Bukoba, ataanza mazoezi kesho.

“Ataanza mazoezi taratibu, yatakuwa ni mazoezi mepesi kwa kuwa ndiyo anaanza,” alisema.

Lipuli FC itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mechi itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba, keshokutwa.

Owino aliwahi kung’ara akiwa na Simba na baadaye Azam FC kabla ya kurejea kwao Uganda.


Beki huyo pia amewahi kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic