SIMBA YAELEZA KIPAUMBELE CHAKE KIKUBWA MSIMU HUU KWENYE LIGI
Na George Mganga
Ikiwa ni siku moja pekee iliyosalia kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambayo ni Jumamosi ya kesho, uongozi wa Simba umesema kipaumbele chake msimu huu si kumaliza ligi bila kufungwa bali ni kuchukua ubingwa.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema kuwa msimu huu wanapigania ubingwa ambao hawajautwaa kwa zaidi ya takribani misimu minne sasa.
Manara ameeleza kuwa suala la kufungwa ama kutokupoteza mechi msimu huu halina maana kuliko kuchukua ubingwa wa ligi wenye maana kubwa kwao.
Simba itavaana na Yanga katika mchezo wa ligi ikiwa kileleni kwa kujikusanyia alama 59 dhidi ya Yanga walio na 48 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment