MAYANJA ATOA UTABIRI WAKE KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA, LIGI KUU BARA
Na George Mganga
Kocha wa zamani wa Simba, Jackson Mayanga amefunguka kwa kwa kueleza mambo kadhaa kuelekea mechi ya watani wa jadi itakayopigwa Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki hii.
Mayanga ambaye aliwahi pia kuwa Msaidizi wa Mcameroon aliyeondoshwa Simba, Joseph Omog, amesema kuwa mechi hiyo huwa haitabiriki kirahisi, japo akisema Simba ina uwezekano mkubwa wa kupata matokeo.
Akizungumza na kituo cha Radio EFM kupitia kipindi cha michezo leo Ijumaa, Mayanja amesema kila aliyejipanga vema basi ataweza kupata matokeo katika mtanange huo unaogusa hisia za watu wengi.
Kocha huyo ambaye yuko Uganda kwa sasa, amezitakia kheri timu zote kuelekea mechi hiyo pamoja na mashabiki wote watakohudhuria Uwanjani kushuhudia mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment