May 7, 2018



Kufuatia kupoteza mchezo wake wa jana katika Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga, uongozi Azam umeeleza sababu iliyopelekea kufungwa.

Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jaffar Idd Maganga, amesema kuwa Azam imepoteza mechi ya jana kutokana na wenyeji kutumia vema faida ya Uwanja wao wa nyumbani.

Maganga ameeleza kuwa Stand walionesha juhudi za kuhitaji matokeo, lakini wamekubali walichokivuna na sasa nguvu zao ni kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons.

Kikosi hocho kinatarajia kuanza safari ya kurejea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic