May 7, 2018



Wakati Wanasimba wengi wakifurahia kuwa na matuamini ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu licha ya kubakiza pinti mbili pekee, Mwanachama Bi Hindu ametofautiana nao.

Mwanachama huyo Mkongwe amewataka mashabiki wote na wanachama wa Simba kuwa na subira kutokana na kwamba ligi haijamalizika, hivyo wasianze kushangilia mapema.

Hindu ameeleza kuwa pointi zilizosalia bado hazijatabirika kama Simba itaweza kuzitwaa au la, hivyo si vema kushangilia mapema.

Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 jana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda FC lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi katika Uwanja wa Taifa.

3 COMMENTS:

  1. Mie nakubaliana na bi Hindi yakwamba Simba ubingwa bado na hakuna haja ya wachezaji kubweteka au wapenzi kuanza kuandaa sherehe. Ukimuua nyoka ili kujiridhisha basi kiondoshe na kichwa chake kabisa. SIMBA ubingwa utakamilika baada ya kuvuna points za michezo yote iliyobakia kwa sababu ligi yetu ina mambo yasiyotabirika unaweza kusikia Yanga akapewa points za Singida kwa kuwa Yondani alitemewa mate nakadhalika nakadhalika. Simba lazima iweke points ziada za hakiba ili kukata mzizi wa fitina.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesema ukweli mkuu, ... hao jamaa wanaweza kupewa pointi za mezani kwa rufaa kwamba kipa wa Lipuli alivaa jezi nyekundu wakati wakicheza na Yanga. Simba inabidi ishinde mechi zote zilizobakia.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic