May 7, 2018



Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Simba kutokea nchini Burundi, Laudit Mavugo, jana aliweka rekodi ya kiaina msimu huu kwa kugusa mpira mara baada ya kuingia kipindi cha pili.

Mavugo aliingia kuchukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi aliyeifungia Simba bao pekee dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi.

Mburundi huyo aliingia Uwanjani zikiwa zimesalia dakika chache mpira kumalizika na kuugusa mpira mara moja pekee, yawezekana ikawa ni wa kwanza kwa upande wa Simba kufanya hivyo tangu msimu huu uanze.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Simba itakuwa inajiandaa na mechi dhidi ya Singida United itakayofanyika mjini Singida kwenye Uwanja wa Namfua.

8 COMMENTS:

  1. Mbona hamsemi aliingia dakika ya ngapi habari hizi wakati mwingine zinatengeneza chuki kati ya mchezaji na washabiki kwani mavugo aliingizwa dakika ya 89 na ziliongezwa dakika nne

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huo ni uandishi wa ajabu sana,mwandishi anajaribu kubalansi stori baada ya upande wa pili kupokea kifurushi cha 4G jana.Mavugo aliyeingia dk.ya 90 hata asingeugusa mpira isingekuwa hoja ya kutoa mtandaoni.

      Delete
  2. Mavugo aligusa mara ngapi pale Stade de 5 juillet 1962?

    ReplyDelete
  3. Na Yanga wameweka rekodi ya kushindwa rufani ya alama za mezani. Huenda watakata rufaa tena kwamba mkuu wa mkoa likuwa mgeni rasmi kwenye ile mechi hhhhhh. Nadhani itakubaliwa this time.

    ReplyDelete
  4. Habari zingine zinaboa Sana, Habari ya kugusa kugusa mpira mpira ndani YA dakika inakuwa issue na siyo ile ya timu ndani YA dakika 90 kushindwa kupata kona hata moja

    ReplyDelete
  5. Habari zingine zinaboa Sana, Habari ya kugusa kugusa mpira mpira ndani YA dakika inakuwa issue na siyo ile ya timu ndani YA dakika 90 kushindwa kupata kona hata moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic