MASHABIKI WANAOINGIA UWANJA WA MAJALIWA KUWAONA SIMBA HUKO LINDI NI BALAA TUPU
Na George Mganga
Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kushuka dimbani jioni ya leo huko Ruangwa Lindi dhidi ya Namungo FC, unaambiwa umati wa mashabiki unaoingia Uwanjani ni mkubwa.
Foleni kubwa ya mashabiki hivi sasa imeshika hatamu tayari kwa kusubiria mchezo huo ambao utakuwa mahususi kwa kuzindua Uwanja wa Majaliwa baada ya matengenezo yake kukamilika.
Ripoti kutoka mji huo zinasema mashabiki wanazidi kumiminika kwa wingi ili kuwaona mabingwa wapya wa msimu wa 2017/18 Simba SC ambao walikosa kwa takribani misimu minne.
Kuelekea mechi hiyo, imeelezwa Simba watashusha mziki wao kamili ili kuwapa burudani wapenzi na msahabiki wake waliopo mjini Ruangwa.
Mech hiyo itakuwa mbashara kupitia kituo cha Azam Sport 2 cha Azam TV.
WAHUSIKA ANZENI KUWEKA TAKWIMU ZETU VIZURI WATU WANGAPI WAMEINGIA UWANJANI, MAPATO KIASI GANI YAMEPATIKANA N.K
ReplyDelete