August 26, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumatatu ya wiki kesho, imeelezwa kuwa mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, atakosekana dimbani.

Simba itashuka kumenyamana na Mbeya City majira ya saa 12 ikiwa ni baada ya kuanza na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi, Agosti 22 2018.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu, Mbelgiji, Patrick Aussems, amesema Okwi atawakosa Mbeya City baada ya kupatwa na majeraha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Agosti 18 2018, Okwi alijitonesha majeraha yake na kushindwa pia kucheza dhidi ya Prisons kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi.

AIidha, kiungo Mzamiru Yassin nayekwenye hatihati ya kutocheza mechi hiyo kutokana na kuandamwa na majeraha.

4 COMMENTS:

  1. Hamna shida mwaka huu mnyama ana kikosi kipana kinachojielewa,watapata tabu sana mwaka huu ngoja ligi ishike kasi.

    ReplyDelete
  2. Simba ya msimu huu hakuna shaka ndani moto nje moto

    ReplyDelete
  3. acha uongo we okwi alipona toka match ya prison na alikuw sub match ya kesho uhakika

    ReplyDelete
  4. Shimba Chi mchezo nje ntiti Ndani ntiti

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic