February 15, 2018


Kiungo mkongwe wa Coastal Union, Athumani Iddi Chuji amesema ameweka rekodi ya kusaidia kuzipandisha timu tatu katika Ligi Kuu Bara.

Chuji amekuwa kati ya wachezaji walioipandisha Coastal Union hadi Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na runinga ya mtandaoni ya Global Tv, Chuji amesema kwake ni rekodi kubwa.

“Nilianza kuipandisha Polisi Dodoma, baada ya hapo Mwadui FC baada ya kuwa nimeondoka Simba na baadaye Yanga.

“Halafu safari hii nimeshiriki kuipandisha Coastal Union. Kwangu ni jambo zuri na ninapenda maisha haya, kufanikiwa kupata ambacho ninakitaka,” alisema.


Chuji alionyesha kiwango kizuri katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara wakati Coasta Union ikishinda kwa mabao 2-0, Chuji akiwa amefunga la pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic