August 20, 2018


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Abeid Mziba, amesema uhakika wa Simba kuetetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao upo shakani.

Mchezaji huyo aliyewahi kutamba katika soka la Tanzania miaka ya 1980 mpaka 1990 amesema kutokana kurejea kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuph Manji anaamini klabu itakaa sawa na kuonesha upinzani mkali.

Yanga imekuwa ikipitia kipindi cha mpito tangu Manji atangaze kuachia ngazi hiyo takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita.

Mbali na ujio wa Manji, Mziba ameeleza namna Kocha wake, Mwinyi Zahera alivyokinoa kikosi na usajili mpya wa baadhi ya wachezaji utaamsha ari na kuleta ushindani kwenye ligi.

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa kundi D uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

15 COMMENTS:

  1. Matokeo wanayopata Simba hayaendani na kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na Mo. Itafika kipindi washabiki wa Simba watakuwa hawaendi uwanjani maana timu walioipa matumaini na kuiamini inawaangusha. Kiwango chao dhidi ya Mtibwa kilikuwa cha ovyo kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu ulitaka iwe inashinda 10-0 ndio uridhike...mpira hauko hivyo kila timu inajiandaa kwa sasa, nakushangaa unaichukulia poa Mtibwa sijui unawaza nini, hujui hao ndio wawakilishi wa Tanzania michuono ya CAF? matokeo ndio jambo la msingi kwa sasa

      Delete
    2. ukweli ndo huo wanahabari waliipamba sana simba tofauti na uwezo wao......simba ya uturuki iliyocheza na mtibwa juzi na yanga ya morogoro iliyocheza na mwarabu jana zina tofauti gani kiuchezaji....au bado mnataka kusema USM sio timu kama mlivyokuwa mnazibeza zile timu za morogoro tulizofanyanazo majaribio?......tukutane tarehe 30/9/2019

      Delete
  2. Unasema nini bwana. Huwezi kuufananisha uwezo wa Manji na ule wa bilionea Mo. Kiwango gani unachokitaka wakati Mnyama ni bingwa na pia kachukuwa kombe dhidi ya Mtibvwa. Na porojo lote hilo ni kwakuwa Manji kenda kuona mechi. Tulia ligi itapoanza na kuona ni timu yako inafanya nini na mnyama anafanya nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usajili wa mabilioni, kambi Uturuki, mishahara ya wachezaji mikubwa balaa, kocha mzungu, halafu mnapata taabu kuvifunga vitimu vya kawaida kabisa. Mtibwa wanacheza na Yanga Jumatano utasikia matokeo.

      Delete
    2. Mamamaeee!!!!.....soon mtapoteana tu.....shughuli ndo imeanza.Mo huwezi kumfananisha na Manji....Mo hela yake iko kibiashara zaidi,anaichungulia,hatoi hovyo,anatoa kibiashara.....Manji ana mapenzi na timu....ni chizi mpira,haoni hasara kubwaga hela akiamua kufanya hivyo.

      Delete
    3. Mbona hushangai team yenye uwekezaji mkubwa kama USM Alger kufungwa na team mbovu maskini kama yanga...alafu nyinyi yanga msijifanye siyo matahira kwani Madrid asumbuliwagi na Gatafe team ndogo...sasa wewe unasemaje Mtibwa katusumbuwa wakati sisi tumeshinda 2-1 na ball possession ilikuwa Simba mwanzo mwisho, wakati wewe umebahatisha kwa mwarabu huku ball possession ilikuwa USM mwanzo mwisho..Alafu acheni kuwa matahira sana Maji jana kaenda kudekea mpira kama mwanachama na siyo M/kiti, Kweli yanga haina thamani wakati Simba Mo anaitaka wanachama hawataki ila kwa yanga imekuwa tofauti wanachama wanataka manji hataki, WAKIMATAIRA mnazingua.

      Delete
  3. Hata huo wakati wa Manji Yanga ilipokutana na Simba Yanga ilitabika sana kupata ushindi zidi ya Simba. Hata ubingwa wake Yanga ulikuwa wa kuungaunga kutoka kwa marefa waliokuwa chini ya Jamali Malinzi aliekuwa mnazi na wanachama halali wa Yanga. Simba licha yaudhaifu wake wakati ule walipambana na kama si uchakachuaji wa ratiba ambao uliwapa mazingira mazuri Yanga hasa kunako mechi za viporo kwa kisingizio cha mechi za kimataifa ili kumchungulia Simba kafikia wapi ili na wao yanga wafanye mabao yao hata ya mizengwe la kama si hivyo basi SIMBA wangekuwa bingwa japo mara moja licha ya Manji wao kuwepo. Simba ilinyanyaswa sana kuanzia kuchukuliwa wachezaji wake kinguvu hadi kupokonywa points ili Yanga ifaidike. Zambi zile ndio chanzo cha matatizo ya Yanga yanayowakabili hivi sasa. Simba kamwe hawamuhofii Manji na kwa kiasi fulani simba wanapendelea kumpiga yanga akiwa katimia. Hata zile tano bila 5:0. Manji aliahidi kuzirejesha na akashindwa licha ya kuwaleta akina Ngoma na wachezaji wengineo wa gharama zaidi lakini hawakufua daku. Mshikamano wa wanasimba ndio siri kubwa ya uimara wa timu yao na sasa Uwepo wa huu udhamini wa uhakika kutoka mwekezaji Mo Yanga waache na kuwa na ndoto za zamani watakuja azirika pale Taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. maelezo mareeeefu lakini point less.....sijaona cha maana ulichoeleza

      Delete
  4. Kweli nimeamin msemo usemao masikini akipata matako hulia mbwata yaani yanga kushinda mechi moja tu mmeanza kejeli za kisenge kiac hiko?usilitukane daraja kabla hujavuka MTO bado,na hats hivyo cc simba tunataka mjiamin hivyo hivyo mpaka siku tunakutana na ninyi ili tuje kuwaibisha vzr na manji wenu huyo vizingizio visije kuwepo simba ndo habar ya mjini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wachezaji wa Simba wanatakiwa wapambane. Wapambane tena washinde kila mechi kwa idadi kubwa ya magoli. Maana kile wanachoonesha uwanjani kwa sasa hakiendani na fedha wanayolipwa.Hatima ya yote utasikia kocha amefukuzwa kwa kutokuwajibika kwa wachezaji. Hayo mambo yalishawahi kutokea Azam wakafukuza karibu timu nzima. Kuna kila dalili Simba inaelekea huko. Ukiangalia ile mechi ya Simba na Mtibwa huoni ile morali inayotakiwa kuoneshwa na mchezaji anayelipwa fedha nyingi. Hilo ni tatizo kubwa.

      Delete
  5. Hii rangi ya Kijani ilipotea kabisa, imekuja kuibuka leo; nina uhakika kwa kiwango kibovu cha yule beki black leo mngetulia na ndiyo maana kocha alimtoa na sidhani kama atabaki pale USM!Lakini bado mtapoteana tu pale Taifa kama mlivyofanya Algeria!

    ReplyDelete
  6. USM hawafanyi vizuri mechi za ugenini hvo sioni ajabu kwa Yanga kupata matokeo,ligi ikianza mambo yatakua hadharani ni jambo la kusubiri tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic