August 20, 2018


Baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga kuwasili Uwanja wa Taifa kuishuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali amesema hana tatizo naye.

Akilimali ameeleza kuwa anamtambua Manji kama mwanachama na si mwenyekiti wa klabu kutokana na kutangaza kuachia ngazi takribani mwaka mmoja na miezi 18 mpaka sasa.

Mzee huyo amesema endapo akimsikia Manji kuwa ametangaza kurejea kwenye nafasi yake kwake hakuna tatizo na atampokea kwa mikoni miwili.

"Mimi sina shida na Manji, najua ameenda Uwanjani kama Mwanachama wa Yanga, endapo akisema anarudi kwenye nafasi yake, mimi sina shida kabisa, namkaribisha" alisema.

Ikumbukwe Manji alitangaza kuachia wadhifa huo kwa sababu alizozieleza kuwa anahitaji muda wa kupumzika pamoja na kufanya masuala yake mengine ya kibiashara.




3 COMMENTS:

  1. Ndumilakuwili. Sasa hapo msimamo halisi wa mzee wenu mnaempamba kila siku ni upi dhidi ya Mwenyekiti wake?
    Mkiwa mnaandika habari msisahau na kukumbushia kilisemwa nini awali ili mtanue soko!

    ReplyDelete
    Replies
    1. hawa waandishi nao sometimes hovyo kabisa.....wanapenda sana kumuhoji huyo mzee wakati wanajua hakuna cha maana anachoongeaga kwa ajili ya maendeleo ya klabu zaidi ya kutengeneza matatizo.......mbona huwa hawaoji kuhusiana na mazuri yanayofanyika hata kama ni machache?

      Delete
  2. Hiki "KINYAGO CHA MPAPURE"shida sana..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic