August 11, 2018


Upo uwezekano mkubwa wa kiungo mchezeshaji wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kutimka ndani ya kikosi hicho kutokana na maelewano mabaya na viongozi wake.

Niyonzima aliyejiunga na Simba msimu uliopita akitokea Yanga, amerejea nchini hivi karibuni akitokea kwao Rwanda, hakuwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, kiungo huyo alitarajiwa kukutana na viongozi wa timu hiyo juzi Alhamisi jioni kwa ajili ya kujadiliana hatma yake Simba. Mtoa taarifa huyo alisema, kiungo huyo ameonekana hana mpango wa kuendelea kuichezea, ni baada ya kutofautiana kwenye baadhi ya makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba.

“Uwezekano wa Niyonzima kubaki kuendelea Simba kwenye msimu ujao ni mdogo kwani yeye mwenyewe ameonekana hana nia tena kubaki kuichezea timu hiyo. “Hata kurejea kwake jijini Dar kumetia hofu ni baada ya kurejea pekee huku familia yake akiiacha nyumbani kwao Rwanda, hiyo inatosha kabisa kuthitibitisha hilo Niyonzima hataichezea Simba katika msimu ujao.

“Kuna baadhi ya vitu ametofautiana na viongozi katika masuala ya kimkataba ambayo wanayafanya siri, hivyo upo uwezekano mkubwa wa Niyonzima kuusitisha mkataba wake Simba na kurejea kucheza soka nyumbani kwao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Niyonzima kuzungumzia hilo alisema: “Sipo kwenye nafasi nzuri kwa kuzungumzia hilo suala katika kipindi hiki, jana (juzi Alhamisi) nilitarajia kukutana na viongozi wa Simba kwa kuzungumza nao lakini hilo halikuwezekana. “Nitalizungumza hilo baada ya kukutana na viongozi wa Simba, kwani kichwa changu hivi sasa hakipo sawa kabisa nafikiria familia yangu ambayo ipo nyumbani Rwanda,” alisema Niyonzima.

CHANZO: CHAMPIONI

8 COMMENTS:

  1. Chama vs Niyonzima

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usifananishe fundi Triple C na uchafu Nyonzima. Ata yeye anajua hana namb ad sasa

      Delete
    2. Hana jpya chama anajua klko yeye

      Delete
    3. WEEEEH CHAMA NI GREDI NYINGINE HUYO. NIYONZIMA AONYESHWE MLANGO WA KUTOKEA AENDE ZAKE. SINA HAKIKA KAMA ATABAKIA TENA TANZANIA MAANA KUSEMA KWELI MPIRA UMEPOROMOKA SANA AMEBAKIA KURUDISHA PASI NYUMA TUUU HAWEZI KUPAMBANA APENYE MBELE HANA UWEZO HUO TENA.

      Delete
  2. Uzuri ligi ya Tanzania huwa haitabiriki hata Tambwe alionekana galasa baada ya kupatikana Mavugo.
    Muda utaamua

    ReplyDelete
  3. ww niyonzima utakuwa umejishitukia kuwa uwezo wako na chama. chama ni zaidi umeogopa usije kuumbuka

    ReplyDelete
  4. Madai gani Niyozima kwa Simba? Timu imemugharamia matibabu nje ya nchi.kuna wachezaji pale Yanga wameumia kipindi na bado wanaendelea kusuasua kupona kutokana na kukosa nafasi aliyoipata Niyozima ya matibabu. Kama kuna madai Niyozima alipaswa kukaa chini na viongozi wake kujadili hayo madai kuliko kususa. Simba imemvumilia Niyozima vya kutosha na kwa kiasi fulani kawatia hasara. Simba wana viungo wa kutosha hivi sasa sioni sababu ya kumbembeleza Niyozima. Ni bora kuelekeza nguvu zao kwingine labda kama tetesi zinazovuma kuwa Simba wamevutiwa na kiwango cha Mbukinafaso wa kotoko basi bora viongozi kuumizwa vichwa vyao jinsi ya kumtwaa kuliko kupoteza muda kwa mchezaji aliepitiliza kiwango cha ukosefu wa nizamu.

    ReplyDelete
  5. Huyu Niyonzima hana shukurani achaneni naye aondoke zake. Hata kama kulikuwa na madai hata kununuliwa pikipiki hapana kumnunulia hana mpira wowote sasa hivi umekwisha amebaki kusumbua vichwa vya watu. AONDOKE . Mchezaji gani msumbufu kila kukicha. OUT.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic