August 21, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha kikao na Waandishi wa Habari leo kunako Makao Makuu yake iliyopo mitaa ya Msimbazi, Kariakoo, Ilala kwa ajili ya kuweka hadharani tarehe ya Uchaguzi Mkuu.

Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ikiongozwa na Mwekezaji Mkuu, Mohammed Dewji 'Mo' jana ilikutana kujadili mambo mbalimbali juu ya uchaguzi huo ambao utafanyika hivi karibuni.

Simba imeamua kutii agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo siku kadhaa zilizopita lilitoa siku 75 kwa Simba pamoja na Yanga kuhakikisha zinafanya uchaguzi ili kupata viongozi wengine watakaokuwa madarakani.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameeleza kuwa leo ataweka kila kitu bayana kwa ajili ya uchaguzi huo pamoja na masuala mengine mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye bodi jana.

Wakati Simba ikiitisha kikao hicho, wekundu wa Msimbazi wataanza rasmi pazia la Ligi Kuu msimu wa 2018/19 kwa kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic