August 21, 2018


Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma ataukosa mchezo wa kwanza ambapo timu itaanza kwa kufungua pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Idd Maganga, amesema kuwa licha ya Ngoma kuanza mazoezi mepesi bado hajawa fiti kwa asilimia 100 kuweza kuanza mechi.

Maganga ameeleza kuwepo uwezekano mkubwa wa mchezaji kukosa mechi kadhaa za mwanzo lakini atakuwa dimbani hivi karibuni akiwashakaa sawa kiafya.

Ikumbukwe mchezaji huyo alisajiliwa kutoka Yanga baada ya kuvunja mktaba wake ambako alishindwa kucheza msimu takribani mzima wa 2017/19 baada ya kuwa majeruhi.

Azam itaanza kibarua cha ligi msimu ujao na Mbeya City kuanza harakati za kuwania ubingwa ambao unashikiriwa na Simba SC waliotwaa msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic