August 21, 2018


Kikosi cha Yanga inashuka rasmi dimbani kesho kutwa Alhamis kuanza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19.

Kuelekea mchezo huo, Yanga imewaomba mashabiki na wanachama wake wapendekeze wachezaji wapi wanapaswa kucheza dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Yanga wameandika wakiwaomba mashabiki na wachama wa timu hiyo kupendekeza kikosi ambacho wangependaa kukiona kinaanza kucheza ili kuridhisha nafsi zao.

"Kesho inaanza ligi kuu Tanzania bara,wewe kama shabiki wa Yanga SC ungependa kikosi kiweje kwenye mchezo wetu Alhamisi?" 

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka hapa nchini, itaanza majira ya saa 10 kamili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

  1. Waandishi kuweni makini hivi yanga anacheza kesho au keshokutwa?

    ReplyDelete
  2. Mashabiki tutakapozoeshwa kupanga kikosi baadae msije mkalalamika kuwa Kocha anaingiliwa kwenye kupanga timu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Timu ileile tuliyocheza na waarabu juzi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic