August 10, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka juu ya fedha za posho ambazo wachezaji wake walipaswa kulipwa baada ya kukipiga na Gor Mahia FC ugenini.

Yanga ilicheza na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika huku ikipoteza michezo yote miwili kwa kufunga jumla ya mabao 7-2.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, ilielezwa kuwa wachezaji wa timu hiyo hawakulipwa posho jambo ambalo imebidi uongozi ulitolee ufafanuzi.

kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya, amesema kuwa hajajua kama walilipwa kwa maana hakuwepo wakati wanaahidiwa.

Aidha Kaaya ameeleza kuwa suala hilo anaweza akalizungumzia Meneja wa timu, Nadir Haroub ili kuweza kulitolea ufafanuzi zaidi kwa maana yeye si majukumu yake.

Wakati Kaaya akitolea ufafanuzi suala hilo, kikosi cha Yanga hivi sasa kipo mjini Morogoro kwa kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Dar es Salaam Agosti 19.

1 COMMENTS:

  1. KATIBU MKUU NDIO KILA KITU WEWE NDIYE BOSI MKUU TAARIFA ZA KLABU LAZIMA WEWE UJUE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic