September 4, 2018


Wachezaji wanne wa timu ya Yanga wameanza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi.

Wachezaji hao baadhi wamejumuika na wenzao kutokana na afya zao kutokuwa sawa baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya rayon Sports uliopigwa Kigalim Rwanda.

Wachezaji waliokuwa majeruhi ni Amis Tambwe, Juma Mahadhi, Papy Tshishimbi, Yusuf Mhilu na Heritier Makambo.

Kurejea kwa wachezaji hao kumeifanya Yanga iimarishe kikosi chake mazoezini kutokana na umuhimu wao ndani ya timu japo bado wengine hawajfanikiwa kuanza mazoezi.

Aidha, Juma Mahadhi na Abdul Juma wao hawakuweza kufanya mazoezi ndani ya kikosi hicho kutokana na afya zao kutorohusu na badala yake wamepewa ratiba ya kwenda kuuguza hali zao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic