Wachezaji hao ambao ni Amis Tambwe, Thaban Kamusoko na kipa Klaus Kindoki walikuwa hawana vibali vya kucheza kwenye mashindano hayo yaliyo chini ya CAF.
Tambwe na Kamusoko vibali vyao vilikuwa vimeshamalizika muda wake huku Kindoki alikuwa bado hajapata tangu asajiliwe na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.
Baada ya kukamilisha ishu ya vibali hivyo, uongozi Yanga umesema mambo sasa ni shwari na watakuwa wanaoneka kwenye mashindano ya kimataifa wakati ujao.
Aidha, Yanga wameeleza kukipata kibali cha kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera ambaye alikaa kwenye mechi dhidi ya Rayon huko Kigali, Rwanda.
Nilidhani mechi na Rayon Sports ndo ilikuwa ya mwisho kwa Yanga... unamaanisha Yanga wataikoma msimu wa 2019/20?
ReplyDelete