September 4, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuripotiwa kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa ameomba kurejea katika timu yake ya zamani, uongozi wa Yanga umekanusha uwepo wa taarifa hizo.

Juzi kulisambaa taarifa mbalimbali ambazo zilisema Chirwa ametuma ujumbe wa sauti akiomba kurejea Yanga kutokana na mambo kuwa mabaya huko Misri alipotimkia kucheza soka lake.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema mpaka sasa hawana taarifa za mchezaji huyo kuomba kurejea hivyo hawezi kuzungumzia kwa kina kilichoripotiwa.

Ten ameeleza kuwa suala la Chirwa kuomba kurejea Yanga lina taratibu maalum ambazo zinahusika kupitia kwenye Kamati ya Usajili na Benchi la Ufundi.

Chirwa aliondoka Yanga baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mwingine ukiachilia wa awali kumalizika.

2 COMMENTS:

  1. Ni jambo lakutia moyo yanga imeanza kuanika ukweli badala ya kukanudha kila kitu na kutangaza yasiyo ya kweli. Mzee Akilimali kaja na siasa mpya ya kuksnusha kila la uwongo

    ReplyDelete
  2. Uliandika huu upumbavu wewe ukisema ametuma ujumbe wa sauti. Mjinga wee!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic