October 22, 2018


Baada ya kuonekana akifanya mazoezi na timu ya Simba B, kiungo Said Ndemla  amefunguka kuwa ameamua kujiongezea dozi ya mazoezi ili kuwa fiti zaidi.

Ndemla amekuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa siku tofauti na wachezaji wengine amekuwa akijifua na kikosi cha Simba B asubuhi uwanja wa Kinesi chini ya kocha Nico Kiondo , jioni amekuwa akijiunga na timu ya wakubwa Uwanja wa Boko Veterani .

"Nimekuwa nikifanya mazoezi na timu ndogo ya Simba pale Kinesi sio tatizo ni jambo la kawaida, huku kwenye timu yangu nako nafanya mazoezi kama kawaida bila shida yoyote na lengo ni kujiweka fiti.

"Na hii inanisaidia kuwa vizuri zaidi kama unavyofahamu soka siku zote ushindani ni mkubwa na unahitaji kuwa imara nyakati zote bila kuzubaa"alisema .

1 COMMENTS:

  1. Ni Jana tu mliandika yakwamba Saidi Ndemla ameamua kwenda au kujishusha kikosi cha pili cha Simba baada ya kuona hawezi kuhimili mikiki ya kikosi cha wakubwa? Kumbe masikini sivyo kabisa ambavyo mtandao huu umeripoti jana na ukweli halisi yakwanini Ndemla anafanya mazoezi na kikosi cha pili. Kumbe ni jitihada zake yeye mwenyewe binafsi Saidi Ndemla kuhakikisha anakuwa fiti zaidi kwa kuamua kufanya mazoezi mara mbili kwa siku baada ya kuona iko haja ya kujipa dozi zaidi ya mazoezi zaidi ya yale anayofanya mara moja kwa siku na kikosi chake cha wakubwa. Waandishi lazima muwe makini na makala yenu kwani mara moja mnaweza kuvuruga kazi nzuri na jitihada za watu wengine kutokana na upotoshaji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic