Kocha mkuu wa Azam FC,Hans Pluijm amesema kuwa
amembadilishia majukumu mshambulaiji huyo akiwa uwanjani kwa kumpa kazi mbili muhimu kutoa pasi ya bao ama kufunga.
Ngoma amecheza michezo mitatu akiwa na Azam FC msimu huu ,tayari ameshatupia bao moja ,alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
"Ngoma ni mchezaji mzuri tangu atoke kwenye majeraha amekuwa akijituma sana,hivyo mimi nimemwambia kuwa kama hatafunga basi atoe pasi ya bao,nina amini atatupa ubingwa msimu huu"alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment