Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba, Laudit Mavungo amesema kuwa kwa sasa yupo huru hivyo anasubiri mkataba kutoka KMC.
Mavugo amesema kuwa amekuwa akisikia taarifa za yeye kuhusishwa kujiunga na KMC kwa muda mrefu hivyo kama wanahitaji saini yake wafuate taratibu.
"Wananiambia kuwa nipo KMC sina mkataba nao hivyo kama KMC wanahitaji huduma yangu wanipe mkataba nisaini kwa kuwa mimi ni mchezaji na uwezo wangu unajulikana na nina uzoefu na ligi ya Tanzania," alisema.
Uongozi wa KMC kupitia kwa msemaji wake Anwari Binde umesema kuwa wamekuwa wakisikia taarifa hizo za Mavugo ila wao wanaendelea na mipango ya kuongeza nguvu kikosi chao.
"Nami nasikia taarifa za Mavugo ila siwezi kuzungumzia kwa sasa maana bado kuna wachezaji tupo kwenye mazungumzo nao tukimalizana tutawajuza," alisema Binde.








0 COMMENTS:
Post a Comment