November 17, 2018


Kuelekea uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani, wanachama mbalimbali wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea.

Katika nafasi ya Uenyenyekiti waliojitokeza kuchukuwa fomu hizo wapo wanne hadi jana Ijumaa ambao ni Jonas Tiboroha, Mbaraka Igangula, Yono Kevele na Titus Osoro.

Kevele na Osoro wao wamechukuwa fomu mbili, ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kila mmoja ambapo Kamati ya uchaguzi imesema watatambua fomu moja pekee itakayojazwa na wagombea hao mara watakaporudisha.

Wajumbe waliojitokeza hadi hiyo jana ni Mussa Katabalo, Salim Seif, Benjamini Jackson, Pindu Luloya, Silvester Haule, Hamad Islam, Shaffii Amri, Said Baraka, Dominic Francis, Ally Msigwa, Leonard Malongo, Salum Chota, Ramadhan Said, Geofrey Mwita, Faustine Mabula, Frank Kalokola na Arafati Haji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic