November 17, 2018


Beki mkabaji wa timu ya Prisons, Salum Kimenya amesema kuwa yupo tayari kucheza katika timu yoyote ambayo inahitaji saini yake kwa kuwa uwezo anao wa kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na Simba ambao wanatafuta saini yake.


Kimenya ambaye pia ni beki wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Starz' amesema kuwa hana wasiwasi na uwezo wake pia mipango ya mikataba yeye mwenyewe anajisimamia hivyo timu ambayo inamhitaji anaongea mwenyewe.


"Mimi najisimamia mwenyewe kwa sasa kuhusu mkataba wangu najua mwenyewe jinsi ulivyo, ila hao Simba waje tu mezani tuongee kisha tufanye makubaliano maana mimi mwenyewe nasimamia maslahi yangu kwa sasa.


"Uwezo wa kufafanua mikataba ninao kwa kuwa natambua vizuri lugha na mpira kwangu ni ajira nacheza kwa kujituma bila kuhofia nacheza na nani mpaka malengo yangu yatimie," alisema.


Katika dirisha dogo kocha wa Simba, Patrick Aussems amewaagiza viongozi wamtafutie beki mbadala wa Shomari Kapombe ili aweze kuongeza nguvu kwenye kikosi chake ambacho kinashiriki michuano ya kimataifa huku habari zikieleza kocha anavutiwa na Kimenya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic