November 5, 2018


Mshambuliaji wa zamani wa LA Galaxy raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 37, huenda yuko njiani kurudi AC Milan kwa mkataba wa miezi sita. (Tuttosport, via Mirror)

Barcelona wameanza mazungumzo na waakilishi wa wing'a wa Chelsea raia wa Brazil William baada ya Chelsea kukataa ofa tatu msimu uliopita. (La Sexta, via Metro)

Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Koscielny, 33, anawindwa na Barcelona, pamoja na mlinzi wa Chelsea raia wa Brazil David Luiz, 31. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chelsea wako mbioni dhidi ya muda ikiwa wangetaka kumsaini kiungo wa kati Mreno Joao Felix, 18, baada ya Benfica kumpa mkataba mpya wenye kipenge cha kuondoka kwake cha kuvunja mkataba cha pauni 105. (Mirror)

Thorgan Hazard, ndugu wa kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard anasema mchezaji huyo wa miaka 27 hawezi kuondoka Stamford Bridge kwenda Real Madrid mwezi Januari. (HLN, via Express)


Arsenal, Chelsea, Liverpool, ­Manchester City na Manchester United huenda wakachukuliwa hatua za kisheria kutoka kwa vilabu vilivyosalia vya Ligi ya Premier ikiwa watajiunga na Ligi iliyopendekezwa ya European superleague mwaka 2021. (iNews)

Wing'a wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 26, ametupilia mbali madai kuhusu hali ya mkataba wake, akisisitiza kuwa yuko na furaha huko Anfield. (Liverpool Echo)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumuacha nje Wing'a raia wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 27, wakati wa mechi kati ya Liverpool na Red Star Belgrade wiki hii. Shaqiri amekuwa akikemewa na mashabiki wa Serbia kutokana na asilia yake ya Kosovo. (Telegraph)


Mlinzi wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand anasema mshambuliajia wa sasa wa Macnhester United Rashfold, 21, anahitaji kuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi ikiwa angetaka kutumia uwezo wake huko Old Trafford. (BT Sport, via Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 33, anasema amekosa sana kucheza na aliyekuwa mchezaji mwenzake huko Manchester United Wayne Rooney, 33, ambaye kwa sasa anaichezea DC United. (Express)

Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti anaamini wachezaji wa PSG Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19, wanaweza kuwa warithi wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. (Express)


Sanamu mpya ya mshambuliaji Liverpool Mohamed Salah, 26, imewekwa nyumbani kwao huko Misri. (Liverpool Echo)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic