November 5, 2018


Na George Mganga

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi maalum wa kujaza nafasi ambazo zilizo wazi ndani ya klabunya Yanga ikiwemo ile ya Mwenyekiti.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea litaanza Novemba 8 hadi 13 2018.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 2019.

TFF wamemua kutangaza rasmi kuanza mchakato huo mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuwataka wausimamie wakieleza kuwa kamati ya Yanga haijitoshelezi.

BMT waliitaka TFF itimize majukumu hayo katika kikao na wanahabari kilichofanyika siku chache zilizopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic