November 19, 2018


Kocha wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23, Bakari Shime amesema kuwa wamejipanga katika mchezo wao wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya timu ya Burundi katika michuano ya Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Shime amesema wanatambua wana deni kubwa la kuweza kupata ushindi ila anaamini watapindua meza kibabe.


"Kazi yetu ni moja tu kupata matokeo kwenye mchezo huo, ushindani ni mkubwa ila kikosi chetu kimeimarika na nimewaambiwa wachezaji waweze kutulia ili kupata matokeo," alisema.


Mchezo wa kwanza  uliochezwa Burundi timu ya Taifa ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri wanapaswa kushinda zaidi ya mabao 2.   

2 COMMENTS:

  1. Kocha SHIME aka SHETANI MWEUSI, Kuwa makini, usije ukayafanya makosa kama aliyoyafanya AMUNIKE alituaminisha hivyo hivyo, matokeo yake akaboronga kupanga kikosi Dhidi ya Lesotho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic