January 20, 2019


Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri ameelezea kuwa vigumu sana kuwashawishi wachezaji wake kufuatia kushindwa na Arsenal.

The Blue ilipoteza 2-0 katika ligi ya Uingereza siku ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates na walikuwa na shambulizi moja pekee lililolenga lango.

Chelsea imeshinda mara mbili pekee katika mechi tano zilizopita na sasa wako pointi tatu pekee mbele ya Arsenal waliopo katika nafasi ya tano na Man United iliopo katika nafasi ya sita.

''Nimekasirika sana kuhusu mwelekeo tuliochukua'' , Sarri alisema. Ni mwelekeo ambao hatuwezi kukubali.

Katika mkutano na vyombo vya habari baada ya timu yake kulazwa, Sarri alisema alitaka kuzungumza kwa lugha ya Kitaliano badala ya Kiingereza kwa sababu alitaka kutuma ujumbe kwa wachezaji wake na alitaka kutuma ujumbe wa wazi.

''Nataka kusema nimekasirika sana, nimekasirika sana'', alisema mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 60, ambaye alimrithi raia mwenzake wa Itali Antonio Conte katika uwanja wa Stamford Bridge.

''Tulishindwa kutokana na mafikra yetu zaidi ya chochote kile. hiki ni kitu siwezi kukubali. Hili kundi la wachezaji hawa ni vigumu kuwasukuma'' alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic