August 12, 2018


Wakati zikiwa zimesalia wiki mbili pekee kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu nchini, baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wamesema ligi hiyo inachelewa.

Mashabiki hao wameeleza kuwa namna kikosi chao kutokana na aina ya wachezaji walionao wanatamani ligi ianze hata leo ili wapate uhondo kamili.

Jeuri hiyo wameipata wakieleza kwa namna usajili wa wachezaji uliofanywa hawaoni timu itakayoweza kuwapa upinzani mkubwa huku wakiamini ubingwa utaendelea kuwa kwao.

Wakati wakitamba kujiamini huko, kikosi cha Simba hivi sasa kipo katika maandalizi ya kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba na Mtibwa watashuka Agosti 18 2018 kwenye Uwanja wa CCm Kirumba, Mwanza kucheza mechi hiyo kisha baada ya siku 3 pazia la ligi litaanza rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic