January 4, 2019




Kocha Ersun Yanal anaamini Mtanzania Mbwana Samatta atakuwa msaada mkubwa katika kikosi chake cha Fenerbahce.

Kati ya wachezaji maarufu waliowahi kukipiga Fenerbahce ni Luis Nani na Robin van Persie.

Fenerbahce ni moja ya timu kubwa nchini Uturuki na Yanal anaamini Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji atakuwa msaada mkubwa kwake na kukikomboa kikosi hicho ambacho kinaonekana kwenda mwendo wa kobe katika Ligi Kuu Uturuki, Toto Super League.

Yanal amesema, Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ndiye chaguo lake namba moja wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Rekodi ya Samatta akiwa na Genk hadi sasa ni mechi 31 akiwa amepiga mabao 21.

Kilichomvutia zaidi kocha huyo ni mechi ya Europa League, wakati Samatta alipopiga mabao mawili na kutoa pasi ya bao Genk ikiishinda Besiktas ambao ni wapinzani wa Fenerbahce kwa maabo 4-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic