UONGOZI wa KMC umesema umejipanga kupambana na JKT Tanzania mchezo utakaochezwa Jumatatu Uwanja wa Uhuru, Jumatatu.
Mchezo huo ambao ulipaswa uchezwe Jumamosi umepelekwa mbele na Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kile walichoeleza ni dharula.
Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema wanatambua uwezo wa wapinzani wao ila kazi yao kubwa ni moja kutafuta matokeo yatakayowaweka nafasi nzuri.
"Kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, tunatambua uwezo wao ni mkubwa hivyo tutakuwa na nidhamu kutafuta matokeo Uwanja wa nyumbani," alisema.
KMC wanashika nafasi ya saba baada ya kucheza michezo 19 kwenye Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi zao 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment