February 20, 2019




BAADA ya safu yake ya ushambuliaji ya Lipuli FC kuwatungua magolikipa wote wa kocha Dragan Popadic wa kikosi cha Singida United Matola leo anainga kwenye kibarua kingine dhidi ya Stand United.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Samora wikiendi hii, Singida United walianza kupata bao kupitia kwa Geofrey Mwashiuya dakika ya 46 na bao la pili dakika ya 84 lililofungwa na Boniphace Maganga.

Bao la kusawazisha la Lipuli lililofungwa na Haruna Shamte dakika ya 61 lilipelekea mlinda mlango, Said Lubawa kutolewa nje dakika ya 62 nafasi yake ikachukuliwa na Ally Mustapha ambaye naye alitunguliwa dakika za lala salama baada ya dakika 90 kukamilika.

Leo Lipuli itakuwa uwanjani CCM Kambarage, mkoani Shinyanga kumenyana na Stand United ambayo nayo ilipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic