USTAA WA SALAMBA WATEKA MAZOEZI SIMBA
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki wa Simba juzi walimvamia kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Mrundi, Masoud Djuma na kuanza kulalamikia aina ya uchezaji wa mshambuliaji wake mpya, Adam Salamba.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi Jumatatu jioni mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kumalizika Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.
Salamba, alisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo hivi karibuni kwa dau la shilingi milioni 40, huku akipewa gari na nyumba ya kuishi akitokea Lipuli FC ya mkoani Iringa.
Kundi hilo la mashabiki walimvaa kocha huyo na kumwambia anatakiwa kukaa kikao na mshambuliaji huyo na kumwambia aache kucheza kistaa kwani bado ana safari ndefu katika soka.
“Tunakuomba kocha ukae na Salamba na kumuonya kuwa yeye bado hajakuwa staa ndani ya Simba, ndiyo kwanza amesajiliwa hivi karibuni hana hata msimu mmoja.
“Katika michuano hii Kagame tumekuwa tukimfuatilia uwanjani akicheza kistaa kama ameshakuwa levo za akina Ronaldo (Cristiano) na Messi (Lionel) kitu ambacho siyo sawa, anatakiwa kubadilika na afahamu yeye bado.
“Kwa sababu ukimuacha aendelee kucheza kistaa mwisho wa siku ataigharimu timu kwa kupata matokeo mabaya, anatakiwa kucheza kwa kupambana kama alivyokuwa Rashid (Mohamed) na Marcel (Boniventure),” alisikika shabiki wa Simba huku kocha huyo akiitikia.
Kocha huyo alimjibu shabiki huyo kwa kumwambia: “Hicho unachokizungumza ni kweli kabisa, mimi nimeliona hilo na kulifanyia kazi na nilikaa naye kikao na kumuonya anatakiwa kubadilika na kuniahidi.
CHANZO: Championi
NI sahihi kabisa. Kujituma uwanjani ni lazima. Wachezaji wetu wanapoteza nafasi nyingi za kufunga magoli kwasababu wanajisahau na mipira inawastukiza.
ReplyDelete