March 2, 2019


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amesema kuwa bado anajiona ni mpya kila siku kwenye soka na ananafasi kubwa ya kuitumikia timu yake katika kuendelea mchakato wa kuutetea ubingwa wa ligi msimu huu.

Chama yupo na timu mkoani Shinyanga ambayo inajiandaa kucheza na Stand United kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa jumapili Uwanja wa Kambarange.

"Kila siku kuna changamoto mpya ambazo zinatokea ndani ya soka, kushindwa kufanya kama jana haina maana kwamba sina nafasi ya kuendelea kutimiza wajibu hapana bado nipo imara," amesema Chama.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Lipuli, Chama aliibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili na ambayo yaliifanya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1  Uwanja wa Samora.

Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 19 ikiwa imejiwekea kibindoni pointi zake 48.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic