March 2, 2019


SUALA la kipa wa Yanga, Beno Kakolanya na klabu yake hiyo, limeingia katika sura mpya kufuatia kupelekwa katika Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ili kupatiwa ufumbuzi.

Kakolanya aliingia katika mvutano na Yanga kufuatia kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera kum­kataa katika kikosi chake kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.

Kutokana na hilo, mlin­da mlango huyo aliomba mkataba wake uvunjwe jambo ambalo Yanga hawakulitekeleza, hivyo kuamua kuliwasilisha suala hilo kwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) chini ya mwanasheria wake, Leonard Richard.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alieleza kuwa suala hilo tayari limeshapokelewa na TFF na sasa lipo kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

“Tumeipokea barua ya Beno hivi karibuni, tayari imewasilishwa katika Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo itaku­tana kwa ajili ya kuli­jadili suala hilo na kufikia ufumbuzi.”

1 COMMENTS:

  1. Jamaa wataendekea kumlipa kila wakijipatia vipesa ijapokuwa hatakiwi nia ni kumkomowa kwa kuuwa kipaje chake na kumzuwia ili asijiunge na Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic