March 2, 2019


Wakati Ligi Kuu Bara ikizidi kushika kasi hivi sasa ikiwa raundi ya pili, inaelezwa Simba wapo katika mikakati ya kumrejesha kiungo wao wa zamani, Ibrahim Ajibu anayekipiga Yanga.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema mabosi wa ngazi ya juu wameanza mchakato wa kumalizana haraka na mchezaji huyo ili aje kuongeza makali kuelekea msimu ujao.

Ajibu mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu na atakuwa huru kusajiliwa na timu nyingine yoyote ile itakayofikiana naye makubaliano.

Ukiachana na taarifa za ndani, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameandika POSTI kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka video ya Mh, Edward Lowassa.

Video ilimuonesha Lowassa akisema ameeudi nyumbani kwa maana ya kutoka CHADEMA kwenda CCM huku Manara akiandika CAPTION iliyosema kuna mchezaji kutoka upande wa pili naye atasema hivyo baadaye.

Maelezo ya alichokiweka Manara Instagram kimetafsriwa kama kuerejea kwa Ajibu kwani ndiye mchezaji aliyetoka Simba misimu miwili iliyopita na kuelekea Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Wakale walisema, Mwenda tezi na homu hurejea ngamani.

    ReplyDelete
  2. Haahaaa...sio Haruna Niyonzima?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic