June 21, 2020


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kiungo wake Said Ndemla anazidi kuimarika kutokana na kufuata maelekezo awapo kwenye mazoezi.

Ndemla hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ambapo iikiwa imecheza mechi 30 yeye amecheza mechi nne.

Jana, Juni 20 alionyesha makeke mbele ya Mwadui FC jambo ambalo limemfurahisha Sven.

"Haya yote ni matokeo ya juhudi ndani ya mazoezi na ndani ya uwanja ndio kitu ambacho ninahitaji kukiona kwa kila mchezaji nina amini kila mchezaji ana kitu chake peke yake hivyo tutazidi kuona uwezo wao ndani ya uwanja," amesema.

Simba ilishinda mabao 3-0 kwenye mchezo huo na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 75 ikiwa nafasi ya kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic