June 21, 2020

YANGA imegawana pointi moja leo mbele ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kasi ya Azam ilianza kipindi cha kwanza ambapo walifunga bao la kwanza kupitia kwa Abdalah Kheri mwamuzi alisema kuwa tayari mfungaji ameotea.

Licha ya timu zote kupambana kwa hali na mali kusaka pointi tatu hakuna aliyepata bao kipindi cha kwanza ambapo timu zote zilikwenda mapumziko ubao ukisoma 0-0.

Tabia ya kujidondosha mara kwa mara kwa mchezaji David Molinga kulimponza kwani alichezewa faulo ndani ya 18 na mchezaji wa Azam FC ngoma ikapeta ikaendelea kama hakuna jambo lililotokea.

Kwa upande wa Azam pia, Nocolas Wadada alichezewa naye faulo ndani ya 18 , mwamuzi hakuamua iwe penalti maisha yakaendelea kusaka pointi tatu.

Dakika ya 48, Wadada alifunga bao kwa upande wa Azam FC lilikataliwa kwa kile mwamuzi alichoeleza kuwa ameotea.

Mbali na Luc Eymael kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Patrick Sibaomana nafasi yake ikachukuliwa na Morrison , Ditram Nchimbi nafasi yake kuchukuliwa na Makame, Molinga nafasi yake kuchukuliwa na Yikpe Gnamien bado mambo yalikuwa magumu.

Kwa Azam FC, Andrew Simchimba aliingia akichukua nafasi ya Richard Djod alionekana kubadilisha mchezo ila bado mambo yalikuwa ni magumu kwa timu zote mbili.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kukusanya poi nti nne mbele ya Yanga ambpo kwenye mchezo wa kwanza, Azam ilishinda bao 1-0 na leo sare inawafanya wasepe na pointi moja.

6 COMMENTS:

  1. Leo Azam kanyimwa goli 2 za dhahiri. Lakini huwezi kusikia waandishi wakijadili kwani timu "yao" ndio imefaidika na uamuzi mbovu wa washika vibendera.

    ReplyDelete
  2. Wamezungumzia zaidi penati ya yanga kuliko magoli ya azam aaliyokataliwa tena tena wamezungumzia juu juu penati iliyokataliwa

    ReplyDelete
  3. Ushauri

    Yanga anzisheni na sio mbaya kuiga utaratibu wa Azam FC na Simba SC ambapo hutafuta mechi ya kirafiki kila baada ya mechi ya ligi iliyoisha ili kuwaweka fiti wachezaji ambao hawakutumika katika mechi ya mashindano iwe ya ligi...Mfano ni kutafuta timu za daraja la kwanza ama la pili na kuwatumia wachezaji wafuatao

    1. Ramadhani Kabwili/Faroukh Shikhalo
    2. Paulo Godfrey/Ally Ally
    3. Adeyum Saleh/Gustavo
    4. Andrew Vincent
    5. Ally Mtoni
    6. Makame
    7. Juma Mahadhi
    8. Banka
    9. Tariq Seif
    10. Raphael Daudi
    11. Erick Kabamba/Mchezaji aliyepandishwa kutokea kikosi cha Timu ya Vijana

    Hii itasaidia kuwaweka fiti ili kuwatumia katika kikosi cha kwanza

    ReplyDelete
  4. Na hatutasikia kelele za kulaumiwa wasmuzi kuwa wamepokea muamala kwa kuwa waluofaidika na hali ya leo ndio mabingwa wa kulalama

    ReplyDelete
  5. Makanjanja wenye timu "yao"kimya.Hamna kelele za kubebwa. Azam wamenyimwa goli mbili za WAZI.

    ReplyDelete
  6. Walizidiwa kwa kila. Tazama jinsi huyo mchezaji wa Jangwani pumzi zimemwishia anavojaribu kumzuwia mchezaji wa Azam anaeelekea kufunga goli kwa kubaka kaputura yake nusuranusura asingemchania na kumuweka pabaya. Wachezaji Hawana fitness wala morali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic