June 21, 2020


FT: Yanga 0-0 Azam FC

Dakika 90 zinakamilika Uwanja wa Taifa

Dakika ya 77 Nchimbi anatoka anaingia Makame
Dakika ya 75 Chilunda anapiga faulo baada ya Mudhathir kuchezewa rafu haizai matunda
Dakika ya 70 Simchimba anaingia anatoka Djod
Dakika ya 68 Yikpe anafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 64 Ngasa anaingia anatoka Balama, Yikpe anaingia anatoka Molinga 
Dakika 60, Idd katoka kaingia Kangwa, Yanga inapata faulo nje kidogo inapigwa na  Morrison inaokolewa
Dakika ya 51 Morrison anapiga kona inaokolewa 
Dakika ya 49 Haule anaokoa mashuti mawili ya Yanga
Dakika ya 45 Morrison anaingia akichukua nafasi ya Sibomana 
Kipindi cha pili kimeanza

HT: Yanga 0-0 Azam FC

Zinaongezwa dakika 2
Dakika ya 45 zinakamilika hakuna timu iliyoona lango
Dakika ya 38 Haule anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 33 Idd anapaisha nje kidogo ya 18
Dakika 31 Fei Toto anafanya jaribio haizai matunda
Dakika ya 30 Yanga wanapiga kona inaokolewa wanapata kona nyingine dakika ya 31 inaokolewa
Dakika ya 24, Metacha Mnata anaokoa mashuti mawili ya Djod ndani ya 18
Dakika ya 21, Molinga anapaisha kichwa angani
Dakika ya 20 Sibomana anapiga faulo baada ya Nchimbi kuchezewa na Idd, inaokolewa na Haule
Dakika ya 15 Molinga anafanya jaribio linaokolewa na Haule, kipa wa Azam
Dakika ya 13 Sibomana anapiga kona ya Kwanza kwa Yanga inaokolewa na Haule
Dakika ya 12 Azam FC wanakosa bao ndani ya 18
Dakika ya 10 Kipagwile anapaisha akiwa ndani ya 18, Azam wanapiga kona ya pili haizai matunda 
Dakika ya 08 Djod anapeleka mashambulizi Yanga
Dakika ya 4 Kheri anafunga bao mwamuzi anadai ameotea
Dakika ya 05 Yondani anampa Kaseke
Uwanja wa Taifa: Yanga 0-0 Azam FC
Kipindi cha kwanza

5 COMMENTS:

  1. Azam wamenyimwa ushindi na waamuzi leo

    ReplyDelete
  2. Kwahakika Yanga hasa kipindi cha pili walikuwa hawajiwezi na kuelemewa vibaya na ni kutokana na kudura ya Mungu ndie aliyewavuwa kipigo na droo hio inwaneemesha wana Msimbazi na ubingwa unapiga hodi za nguvu. Jee mambo yangekuwa vipi Lau wana Lambalamba wangekuwa kamili?

    ReplyDelete
  3. Utopolo pumzi imekata. Refa na wasaidizi wake wamemeza goli mbili dhahiri.Angalia Azam TV baadaye kwa ushahidi. Two clear goals.

    ReplyDelete
  4. Wamezoea kusema Simba wanabebwa leo sijui wataandikaje na magazeti yao

    ReplyDelete
  5. Makanjanja watauchuna. KWANI timu yao imefaidika na uamuzi mbovu. Zile goli 2 zilizokataliwa ingekuwa dhidi ya Simba ripoti ingepelekwa mpaka bungeni.Waandishi wa michezo wa Tanzania ovyo kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic