March 7, 2021


 LICHA ya nyota wao Fiston Abdulazack, kupachika bao la kuongoza kipindi cha kwanza dakika ya 41 halikuwafanya Yanga kusepa na pointi tatu, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Fiston alipachika bao hilo la kwanza kwa kisigino mbele ya Kelvin Yondani ambaye aliamini kwamba nyota huyo ameotea ila mwamuzi Mwinyimkuu Abdalah aliweka mpira kati.

Mpaka dakika 45 zinakamilika ubao ulikuwa unasoma Polisi Tanzania 0-1 Yanga na kuwafanya vinara hao wa ligi kuingia kipindi cha pili kwa kujiamini.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote mbili zilikuwa zinashambuliana kwa zamu na iliwabidi Polisi Tanzania wasubiri mpaka dakika ya 89 kupachika bao la kuongoza.

Ilikuwa ni kupitia kichwa cha Pius Buswita ambaye aliweka mzani sawa kwa mpira wa faulo ya Cosmas na kuizamisha mazima nyavuni.

Licha ya kuwa walikuwa pungufu Polisi Tanzania kwa kuwa beki wao kisiki Kelvin Yondani alionyeshwa kadi mbili za njano na kufanya aonyeshwe kadi nyekundu.


Sare hiyo inafanya Polisi Tanzania kufikisha pointi 29 ma ipo nafasi ya nane huku Yanga ikiwa na pointi 50 imecheza jumla ya mechi 23. 

Pia kikosi cha Yanga leo kilikuwa na mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kurejea kwa nyota wao Ditram Nchimbi ambaye alikuwa anapambana na timu yake ya zamani ya Polisi Tanzania.

6 COMMENTS:

  1. Pius Buswita alifunga kwa kichwa mbele ya Bakari Nondo Mwamnyeto.... Ungeandika hivyo ingependeza zaidi

    ReplyDelete
  2. Ni matokeo ya mpira. Point 3, 1 au 0

    ReplyDelete
  3. Shughuli ipo kwa upande wa yanga kwakua Simba ni dhahiri anarejea kwenye usukani wa ligi kwakua Ana mechi 4 mkononi jahazi limezama

    ReplyDelete
  4. Kiukweli kocha wa yanga kaishiwa mbinu au nizar khalifan aondoke aletwe msaidizi mwngne unaonekana hawana mbinu za kutosha subirini mnyama amalize viporo vyake

    ReplyDelete
  5. Tangu izaliwe yanga miaka 85 iliyopita haikuwahi kutumia mabilioni kwa kununulia mastar wenye sifa zao ambao wengi ambao ni wachezaji wa timu zao za Taifa lakini ni jambo la kudikitisha wameishindwa kuitendea mema timu yao. Hapo wapime kujuwa sababu ili wajirekebishe

    ReplyDelete
  6. Mbona hamuandiki kaze kafukuzwa? Au mmelala

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic