April 17, 2021


 BEKI wa kati wa Simba, Muivory Coast, Pascal Wawa ameibuka na kuweka wazi kuwa kutokana na ubora wao kwa sasa haoni atakayeweza kuwazuia kutetea ubingwa wao msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

 

Wawa ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Wawa amesema: “Nadhani bado tupo kwenye ubora ndiyo jambo kubwa la kumshukuru Mungu kwa sababu licha ya ushindani na ugumu wa ligi lakini bado tumekuwa na uwezo wa kupata matokeo bora zaidi kwa upande wetu.

 

“Kiukweli naamini nafasi ya kutetea ubingwa wetu ipo wazi na hakuna ambaye anaweza kuzuia hilo kwa sasa kutokana na kuwa kwenye kiwango bora cha ushindani, kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kushinda mechi zetu ili malengo yatimie bila ya kuangalia nani anaongoza ligi,” amesema Wawa.


Simba imekusanya pointi 49 ikiwa nafasi ya tatu na imecheza mechi 21 huku vinara wa ligi wakiwa ni Yanga wenye pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.


Leo Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa na Simba kesho itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Karume.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic