April 17, 2021


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi amesema kuwa anaamini kwamba atafunga kwa kuwa anaumizwa kwa kukaa muda mrefu bila kufunga.

Nchimbi msimu huu wa 2020/21 Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 na kukusanya jumla ya pointi 51 hajafunga hata bao moja.

Timu yake ikiwa imefunga mabao 37 amehusika kwenye mabao mawili ambapo alitengeneza pasi za mwisho.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United na huenda akaanza kwenye kikosi cha leo kwa sababu mchezo uliopita dhidi ya KMC alianzia benchi.

Nyota huyo mzawa amesema: "Ninajua kwamba sijafunga siku nyingi hilo lipo wazi na ninamuia kwa kuwa nijafunga, hilo sio jambo jema kwangu.

"Kwa sasa ninaamini kwamba mvua zikianza kunyesha huwa ninafunga, nikipata nafasi ninaamini nitafunga, mashabiki wasiwe na mashaka tutafanya vizuri," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic