UONGOZI wa Klabu ya Simba leo Aprili 20 umeingia makubaliano ya kimkataba na mfanyabiashara maarufu Bongo, Fred Vunja Bei kwa ajili ya kuuza bidhaa za timu hiyo.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuendelea kutoa ajira kwa vijana kama ilivyokuwa sera ya Hayati, John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano na sasa chini ya Samia Suluh ambaye anaendeleza kuiongza Tanzania baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki.
Barbara amesema kuwa wengi waliomba tenda kwa ajili kuingia makubaliano na Simba ila mwisho wa siku wamempata Mtanzania, Vunja Bei.
"Ilikuwa ni wengi waliomba tenda ya kufanya kazi na Simba ila tunafurahi kusema kuwa Vunja Bei ambaye ni Mtanzania ameshinda tenda hiyo.
"Atakuwa na kazi ya kusambaza bidhaa za Simba kila mahali nchini Tanzania na kutakuwa na mobile shop ambazo zitakuwa kila mahali, hata kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar pia atakuwa anasambaza bidhaa zetu.
"Bidhaa za Simba ikiwa ni kuanzia barakoa, jezi na vyote vitakavyokuwa ni vya Simba basi vitakuwa vinapatikana," alisema.
Vunjabei amesema kuwa anafurahi kufanya kazi na Simba na kupewa mamlaka ya kusambaza bidhaa hizo jambo ambalo atalifanya kwa uaminifu.
IGA ufe
ReplyDeleteIGA ufe
ReplyDeleteNdio!tunaweza!
ReplyDelete