June 20, 2021


WAKATI leo Juni 20 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu dhidi ya Mwadui FC, kuna hatihati ya kuwakosa nyota sita kutokana na sababu mbalimbali. 

Nyota hao ni Metacha Mnata kipa namba moja wa Yanga huyu amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu kwa muda usiojulikana.

Farid Mussa, Mukoko Tonombe hawa bado hawajawa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Lamine Moro nahodha wa Yanga, Michael Sarpong na Wazir Junior hawapo kwenye mpango wa Nabi.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wao uliopita walipokutana Uwanja wa Kambarage, ubao ulisoma Mwadui 0-5 Yanga.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 30 kibindoni ina pointi 64 inakutana na Mwadui FC ambayo ipo nafasi ya 18 na pointi 19.

5 COMMENTS:

  1. Mwadui ni wateja wa Utopolo kwahiyo hata wakikosekana wachezaji kumi wa kikosi cha kwanza hakuna shida

    ReplyDelete
  2. Leo wakishinda Matopolo hata kwa goli moja tu hstutopata PA kukaa kwa sherehe za ushindi na tamaa upya ya ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic